Find Us On Facebook
 
X

Tuesday 14 January 2014

UTABIRI MPYA WA KUTISHA-MWISHO WA DUNIA WATAJWA

Stori: Mwandishi Wetu na Mitandao
WAKATI binadamu wakiendelea na
mipango yao ya kuifanya dunia kuwa
sehemu salama ya kuishi kimazingira,
kiulinzi na usalama, utabiri mpya wa
kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032
ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu katika
mfumo wa jua.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali katika
mitandao ya internet, sayari iitwayo
Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika
kama Planet X ipo njiani kuigonga dunia
na hivyo kusababisha majanga mbalimbali
kutokea.
ITAONEKANA ANGANI KAMA MWEZI
Kwa mujibu wa mitandao hiyo ya
kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea
dunia kwa kasi kubwa, itaonekana kubwa
na angavu wakati wa usiku angani na
kuwa katika umbo la mwezi na hivyo
kufanya miezi ionekane miwili.
DALILI KWAMBA IPO JIRANI
Taarifa zaidi za kisayansi zinasema kuwa,
kadiri sayari hiyo inavyozidi kusogea,
dunia itaanza kutikisika na kusababisha
matetemeko ya ardhi kuongezeka sehemu
mbalimbali.
Mbali na dunia kutikisika na matetemeko,
milipuko ya volcano nayo itatokea huku
idadi kubwa ya milipuko hiyo mipya
ikiongezeka, vimbunga vikubwa kama
Tsunami vitaibuka na mwishowe dunia
itapigwa na bomu la miamba midogo na
vimondo kutokea angani.
DUNIA ITAKUMBWA NA GIZA NENE
Wakati volcano zote duniani zitakapoanza
kulipuka na zingine mpya kujitokeza,
dunia itafunikwa na giza nene na matope
kwa wakati wote wa usiku na mchana
huku watu wakitakiwa kusoma katika
Biblia Joel 2: 1-2 na Zephaniah 1:14-17.
NI TUKIO LA AINA YAKE KARNE YA 21
Nibiru inatajwa kama kitu kinachoisogelea
dunia kinachoaminiwa kusababisha
madhara makubwa ambapo kama
hakitaigonga dunia, kitasababisha
mtikisiko usio wa kawaida
kitakapopishana nayo. Baadhi ya
wanasayansi wanaamini kuwa kitendo
hicho kitatokea mapema katika karne ya
21 (tuliyonayo sasa).
WANASAYANSI WAPINGANA
Baadhi ya wanasayansi wanapinga kwa
maelezo kwamba hakuna ushahidi
wowote wa kitafiti unaoonesha wazi kwa
mabingwa wa anga za juu waliobobea wa
masuala ya nyota.
MWANAMKE ALIWAHI KUOTA NDOTO
Kwa mara ya kwanza jambo hilo lilitokea
mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy
Lieder muasisi wa mtandao wa ZetaTalk,
aliwahi kudai kuoteshwa ndoto kwamba,
Mei 2003 kuna kitu kitaingilia mfumo wa
jua (solar system) na kusababisha dunia
kutoboka tundu litakalosambaratisha
sehemu kubwa ya kizazi cha binadamu.
Lieder aliifafanua kuwa, kitu hicho
kitakuwa na ukubwa wa mara nne ya
dunia.
BAADA YA NDOTO
Baada ya mwanamama Lieder, mtu wa
kwanza kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark
Hazlewood, mwanachama wa zamani wa
mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001
alichapisha kitabu kilichoitwa Blindsided
na kusema kuwa mwisho wa dunia
ungekuwa mwaka 2003 baada ya kuwasili
kwa sayari ya kumi (Nibiru).
Katika mfumo wa sasa, baadhi ya
wanasayansi wanasema sayari ziko 12,
wakizitaja kwa namba 1. Jua 2. Mercury 3.
Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi) 6. Mars 7.
Jupiter 8. Saturn 9. Uranus 10. Neptune
11. Pluto 12. Nibiru.
IMANI NYINGINE YASEMA MWISHO WA
DUNIA NI FEBRUARI 22, 2014
Hata hivyo, utabiri mpya uliotolewa na
watu wa jamii ya Vikings jijini New York,
Marekani umesema mwisho wa dunia ni
Februari 22, mwaka huu.
Mitandao mbalimbali pamoja na gazeti
maarufu la Daily Mail la Uingereza
lilielezea utabiri huo uliofanywa na jamii
hiyo ukidai kuwa mwisho wa dunia
utatokana na Mungu Odin kupigana na
kuuawa na shetani Wolf Fenrir, hivyo
kuiachia dunia anayoishikilia.
Wamesema baada ya kuiachia dunia
itafurika maji ambayo yatakuwa na sumu,
hivyo viumbe wote watateketea.
WATUMISHI WA MUNGU TANZANIA
Baadhi ya watumishi wa Mungu nchini
wamekuwa wakisimamia andiko la kwenye
Biblia linalosema kuwa, hakuna
mwanadamu anayeijua siku wala tarehe
ya mwisho wa dunia na ni siri ya
Muumba.
Makanisa mengi nchini Tanzania yana sera
tofauti lakini yanaongozwa na Biblia
moja. Makanisa hayo ni Romani Katoliki,
Lutheran (KKKT), Anglikana na makanisa
ya kiroho kama Full Gospel& Bible
Fellowship la Zakaria Kakobe.
FREEMASON WABARIKI
Jamii ya Freemason tayari imebariki
mwisho wa dunia kwamba umefika na
dunia inatarajie tukio kubwa la pamoja.
Mitandao ya jamii hiyo inataja kama hizi
ni nyakati za mavuno kwa maana kwamba,
upande wa Mungu na shetani
kushindania watu huku waendao
upotevuni wakiwa wengi.
MFUMO WA DUNIA TANGU KUUMBWA
Kwa mujibu wa kitabu kinachoitwa
Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu
kuumbwa kwake umekuwa na matukio
makubwa kila baada ya miaka 2000
(inaweza isitimie au ikapita kidogo).
Tangu kuumbwa kwa Adamu na Eva
mpaka gharika inadaiwa ni miaka 2000.
Gharika hadi dunia kubadili mfumo wa
mawasiliano (Mnara wa Babeli) ni miaka
2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi saa ni
miaka 2000 ambapo katika karne hii,
dunia huenda ikaingia katika tukio kubwa
sana ambalo halijawahi kutokea.
Source:Global publishers

0 comments:

Post a Comment