Find Us On Facebook
 
X

Tuesday 21 January 2014

SIRI NZITO KWA WAKINADADA...!!! UKITUMIA NJIA HIZI 18 NAKUHAKIKISHIA UTADUMU NA MWANAUME WA AINA YEYOTE HAPA ULIMWENGUNI..SOMA HAPA KUIJUA SIRI HII

 
I was single once, but now i'm a wife and a
mother. Nimekaa nikaona sio vibaya iwapo
nta-share tips kadhaa zilizonisaidia kumuweka
baba watoto sawa na mpaka leo hii sijawahi
kuhisi wala kugundua kwamba anatoka nje ya
ndoa yetu, japo matatizo ya hapa na pale
hayakosekani ila tumedumu na bado
tunaendelea na safari.
Unapokutana na mwanaume akakutongoza/
mwanamke akakukubalia kuna uwezekano
mkubwa kuwa amevutiwa na wewe kweli au
kakutamani tu. Kitu ambacho watu hua
wanasahau ni kwamba hata mtu aliyekutamani
tu unaweza ukampa mwongozo/sababu mpaka
mwenyewe akajikuta anakupenda kuliko
ambavyo angeweza kutarajia kwamba angewahi
kupenda. Ndio maana hata wale waitwao 'bad
girls/boys' hua wanajikuta wamenaswa na
kunasika at some point.
1. Usiigize.
Maigizo waachie wasanii wetu, kuwa vile
ulivyo kweli kimaisha/kitabia (isiwe mbaya)/
mazoea n.k
2. Don't move too fast/act desperate.
Usitumie ule muda wa mwanzo kabisa wa
mahusiano yenu kutaka kujua "una malengo
gani na mie?" "utanioa?" "Kanitambulishe/
nataka nikakutambulishe." n.k Mpe nafasi ya
kukusoma na kupata kujua wewe ni mtu wa
aina gani, je unafanania na mwanamke ambae
angependa kuwa nae kwa muda mrefu,
possibly hata ndoani? Na wewe nawe tumia
muda huo kufanya kitu hicho hicho.
3.Don't be too demanding.
Huyo sio baba yako wala sio mume just yet,
hivyo chochote atakachokufanyia kinatokana
na yeye kutaka/kupenda kufanya hivyo na sio
kwakulazimika. Haki hiyo hauna.
4. Kuwa na shukurani.
Learn to appreciate all that he does for you,
that way ataona umuhimu wa hayo
anayokufanyia, yawe makubwa au madogo.
5. Be real.
Badala ya kufika kwake na kuanza kushangaa
anaishije bila ya mfanyakazi wa ndani huku
ukitamba kuwa wewe huwezi, shangaa
anawezaje weka nyumba yake katika hali nzuri
mwenyewe bila ya msaada. Hii itaonyesha fika
wewe utakua mke wa aina gani hapo baadae,
kama ni wale wakukaa miguu juu huku
wakiagiza hata maji waliyoombwa na mume au
la.
6. Learn to cook if you don't know how to.
Waliosema "the way to a man's heart is
through his stomach" hawakukosea. Ukiachilia
mbali wale watu wachache wanaokula ili
kushiba wengi hua wanajali ladha. Hiyo ndio
hua inawaongezea hamu ya kula na
kuwarudisha nyumbani mapema pia
kuwafanya wakumiss pale inaposhindikana
kula chakula chako . Kwakumwonyesha
mwanaume kwamba hata tumbo lake unaweza
kuliridhisha unamwongezea sababu za
kukuweka kwenye maisha yake.
7. Mheshimu.
Mpe heshima yake kama mwanaume wako ila
usimwogope. Wengine wote usiwape nafasi
kumfanya ajisikie kwamba haheshimiki.
8. Kuwa ngao yake.
Inapotokea anakumbwa na matatizo yoyote
yale onyesha utayari wa wewe kuwa pamoja
naye kwa hali na mali mpaka yatakapoisha. Pia
usikose kumjali kumpa moyo pale unapoona
inahitajika.
9. Kuwa muwazi.
Kama kuna mambo ambayo unajua moja kwa
moja yatakuwa sehemu ya mahusiano yenu
(watoto/X mkorofi .nk) mweleze mapema ili
aamue kama yuko tayari kudeal nayo au la.
10. Usiwe na chuki.
Kikifika kipindi cha yeye kukutambulisha kwa
ndugu na rafiki zake onyesha ushirikiano.
Usionyeshe chuki wala kujiona kana kwamba
wewe ndio wewe.
11. Give your all.
Kama na nyie mtaamua kuonjeshana tunda
kabla (kama ambavyo wengi wanafanya karne
hii) basi kuwa mbunifu, mtundu na usiwe
mvivu.
12.Pendeza.
Vaa/onekana vizuri unapokuwa nje hata ndani
pia. Usisahau kuzingatia/jali hisia zake kuhusu
mavazi
yako.
13. Onyesha interest kwa yale ayapendayo
yeye.
Usiwe mbinafsi kila siku unataka kusikilizwa
wewe tu na story/mambo utakayo wewe.
Uliza/jua kuhusu yale anayopenda yeye mf.
mpira/siasa.
14.Kuwa mtulivu.
Usiwe mtu ambae kila saa simu yako inapigwa
pigwa na wanaume wasio ndugu wala marafiki
wakaribu na wanaoeleweka. Discpline ni
muhimu sana.
15.Usimzonge.
Usiwe mmoja wa wale watu wanaofuatilia
wenzi wao masaa yote wanapokuwa hawapo
pamoja. Mpe nafasi ya kuwa na marafiki zake
bila kuhitaji kuzima simu ama ku-ignore simu/
text zako.
16. Mfurahishe/chekeshe.
Joke around sio muda wote yeye ndio awe
wakukufurahisha wewe.
17. Jifunze kusamehe.
Mambo madogo madogo yanapoombewa
msamaha samehe na uache yapite.
18. Mshirikishe Mungu wako.
Ukishaona kwamba huyo ndie basi mshirikishe
yule unayemwamini ili upate mwongozo wa
kiroho.

0 comments:

Post a Comment