Lionel Messi hatoandoka Barcelona kujiunga na Paris Saint-Germain au
klabu nyingine yoyote katika kipindi cha hivi karibuni, baba na wakala
wa mwanasoka huyo bora wa dunia kwa mara nne mfululizo amesema.
Matajiri wa Paris wamekuwa wakiripotiwa kuandaa ofa ya rekodi ya
dunia ya kiasi cha €250 million wakati wa dirisha kubwa la usajili ili
kumleta staa huyo wa Barca katika Ligue 1.
Hata hivyo, Jorge Messi amekanusha taarifa hizo zinazosema kwamba
mwanae ataenda Paris kutoka Camp Nou na kusema Messi hatoondoka Barca
hivi karibuni.
“Nimesikia kuhusu tetesi hizo na sijui wapi zinatoka,” Jorge Messi aliliambia gazeti la L’Equipe wakati alipoulizwa taarifa kuhusu PSG.
“Hakuna chochote mpaka sasa. Lionel ni mchezaji wa Barcelona, ambapo ana mkataba kwa miaka kadhaa ijayo mpaka 2018.
“Ni heshima kujua PSG wanamfikiria yeye, lakini narudia tena hilo suala sio moja ya vitu tunafikiria kwa sasa.
“Ukweli pekee ni kwamba ana mkataba na Barca. Hatutaki kufikiria
kuhusu timu nyingine aidha Paris au timu nyingine yoyote kwa sasa.”
Monday, 27 January 2014
MESSI HATOJIUNGA NA PSG AU KLABU YOYOTE HIVI KARIBUNI.” ASEMA BABA YAKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment