Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi
(mbele ya basi lililopinduka aliyenyoosha mkono) akiangalia basi la
Shabiby lililopinduka eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida.Basi
hilo ambalo lilijeruhi abiria 28 akiwemo kondakta aliyevunjika miguu
yote, lilipinduka katika harakati zake za kulipita basi jingine.
Lori la mafuta lililogongwa na basi la Shabiby na kusababisha abiria 28 kujeruhiwa.
Kondakta
wa basi la shabiby Tadei Mhando aliyevunjika miguu yote miwili baada ya
basi hilo kupinduka eneo la kijiji cha Kisaki manispaa ya Singida.
Waauguzi wa hospitali ya mkoa mjini hapa,wakimpeleka kondakta Tadei
Mhando chumba cha upasuaji.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
ABIRIA 48 wa basi la kampuni ya
Shabiby lifanyalo safari zake kati ya mkoa wa Arusha na Dodoma,
wamenusurika kufa baada ya basi hilo kupinduka wakati likijaribu kupita
basi jingine.
Basi hilo aina ya Yutong lenye
namba za usajili T.930 BUW, limepinduka katika barabara kuu ya
Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Kisaki Manispaa ya Singida.
Ajali hiyo imetokea Januari 13 mwaka huu saa saba mchana wakati basi hilo likitokea mkoani Arusha kuelekea mjini Dodoma.
Kondakta wa basi hilo,Tadei Mhando
amesema kati ya abiria hao,28 wakiwemo watoto wawili,wamepata majeraha
katika sehemu zao mbalimbali za miili yao.
“Mimi ndiye niliyeumia zaidi kuliko
majeruhi wote wa basi letu.Nimevunjika miguu yote miwili na sasa
natarajia kuingizwa ‘theater’ kwa matibabu zaidi.Tunashukuru hakuna mtu
aliyepoteza maisha”,amesema Tadei.
Akifafanua zaidi juu ya ajali
hiyo,Tadei amesema walipofika eneo la tukio la Kisaki ambalo lina
mwiinuko huku basi lao likiwa kwenye mwendo kasi,dereva wao alijaribu
kulipita basi la princess Muna.
Amesema katika jaribio hilo,mabasi
yote mawili yakawa kwenye mwendo kasi unaofanana na wakati huo huo,lori
la mafuta lililokuwa linapishana na mabasi hayo,liliibana basi la
shabiby na kusababisha ligonge lori hilo ubavuni karibu na kichwa.
“Kutokana na kubanwa huko huku
Shabiby likiwa kwenye mwendo kasi,dereva alishindwa kulimudu na hivyo
kusababisha lipinduke na kuharibika vibaya”,alifafanua Tadei.
Mkuu wa wilaya ya Singida,Queen
Mlozi na kamati yake ya ulinzi, ilifika hospital ya mkoa na kuwapa pole
na majeruhi na kisha alienda eneo la tukio Kisaki.
CHANZO: MOBLOG
CHANZO: MOBLOG
0 comments:
Post a Comment