Find Us On Facebook
 
X

Wednesday 22 January 2014

NAY WA MITEGOAZUNGUMZIA JUU YA YEYE KUMUUNGA MKONO LOWASA KUELEKEA UCHAGUZI 2015


Hitmaker wa ‘Nakula Ujana’ Nay Wa Mitego amesema anatamani kumuona Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akigombea Urais 2015,huku akiahidi kumuombea katika mamlaka husika ili agombee.
Nay
Akizungumza  leo Nay wa Mitego amesema baada ya kumuimba Lowassa katika wimbo wake Salamu Zao, amepokea maoni kutoka kwa vijana kuwa Lowassa ndiye kiongozi atakayeifaa Tanzania.
“Nikizungumzia kuhusu Lowassa yaani kila mtu anam-support,kwasababu hata ukiangalia comment za kwenye Instagram kila mtu anamadmire. Mimi sio mwanasiasa na wala siwezi siasa lakini ni mtu ambae namkubali sana .Mimi namkubali sana na kama ikiwezekana tukatuma maombi pia awepo kwenye wagombea Urais wa 2015,sijui kama yeye yupo na plan hiyo lakini vijana na mimi tumetokea kumwelewa sana na nimegundua watu wengi wapo nyuma yangu,”amesema Nay wa Mitego.

0 comments:

Post a Comment