Find Us On Facebook
 
X

Wednesday 22 January 2014

HAYA NDIYO MAJIBU YA MWIGULU NCHEMBA KWENDA KWA WANAOPONDA UTEUZI WAKE,AWEKA WAZI ELIMU YAKE

Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha, Mwigulu
Nchemba, ambaye jana alikuwa miongozi mwa
manaibu waziri walioapishwa na Rais Jakaya
Kikwete kushika nyadhifa zao amewaambia
watu wanaoponda uteuzi wake kuwa hana haja
ya kubishana nao kwani hawamjui.
Katika maelezo yake, Mwigulu alisema
anamshukuru Mheshimiwa Rais kwa
kumwamini kuwa anaweza kumsaidia katika
kusimamaia sera na mipango ya fedha nchini.
Watu wasionifahamu wanadai mimi sina
viwango vya kufanya kazi hii; naomba
wafahamu kuwa mimi ni msomi mwenye
shahada ya ya pili ya uchumi na hivi sasa niko
katika masomo ya kupata shahada ya uzamivu.
Mwigulu aliendelea kusema “Kabla sijaingia
kwenye siasa nilikuwa nafanya kazi katika
Benki Kuu ya Tanzania kama mchumi.
Ninakwenda Wizara ya Fedha kusimamia
mambo manne ambayo ni uadilifu,
ushirikiano, jitihada na huduma madhubuti
ambazo zitatolewa kwa wakati mwafaka.

0 comments:

Post a Comment