Meli hiyo itajengwa na kampuni ya China Shipbuilding Industry
Corporation na itatumika kupamba park ya kaunti ya Daying iliyopo
Sichuan kwa kuegeshwa kwenye mto Qi nchini China.
Meli hiyo haitatumika kusafirisha abiria na watalii kwenye kina kirefu
cha bahari kwakuwa si watu wengi wanaweza kuingia tena kwenye safari ya
kufanana na Titanic ambayo haikukamilika. Badala yake meli hiyo itakuwa
alama ya mzuka wa Titanic.
Shirika la habari la Xinhua limesema meli hiyo itatengeneza hali
ilivyokuwa pale meli hiyo ya kufahari ilipogongana na mwamba wa barafu.
Ujenzi wa meli hiyo yenye urefu wa meta 270 unatarajia kumalizika baada ya miaka miwili.
Hii si mara ya kwanza kwa watu kutaka kutengeneza meli nyingine ya
Titanic. Bilionea wa Australia, Clive Palmer alitangaza kutengeneza
‘Titanic II’.
Source:-Bongo5.com
Source:-Bongo5.com
0 comments:
Post a Comment