Mh. Frederick Sumaye akihojiwa na Maestro wa Sports Extra ya Clouds FM picha ikiwa imepigwa na http://michuzijr.blogspot.com ambapo kwenye Exclusive interview Frederick Sumaye ndio ameyatoa yake ya moyoni hapa chini.
1. ‘Tatizo langu la kwanza ni
kwamba tumewafikisha Watanzania mahali ambapo tunafikiri wakipata katiba
mpya ndio jawabu la matatizo yao, ukiangalia sana watu waliokua wakitoa
maoni hatukuwapa elimu ya kutosha juu ya katiba kwa hiyo walikua
wanaeleza machungu wanayoyapata kwenye maisha wakifikiri yanasababishwa
na katiba hivyo ikipatikana mpya haya yatatoweka kitu ambacho sio kweli’
2.’Katiba mpya haitatatua
matatizo yao kama wanavyofikiria, kitakachotatua matatizo yao ni
usimamizi mzuri wa sera na sheria zetu, kama tutasimamia vizuri hayo
hata kama katiba ingekua ya karatasi moja nchi bado itakwenda mbele’
3. ‘Katiba hata ungeitengeneza
leo……. baada ya miaka mitano, miwili au mitatu itaanza kuwa na
marekebisho kwa sababu jamii haijaganda.. katiba zile ambazo
hazibadiliki sana duniani kama ukizichunguza ni zile ambazo haziweki
kila kitu kwenye katiba yani kama kuna mabadiliko kwenye jamii ni sheria
tu zinabadilika ila katiba inabaki palepale’
4. ‘Na neno viraka sio sahihi, hili ni neno tu ambalo linatumika na wale ambao hawaitaki katiba hii kwa sababu yeyote’
5. ‘Katika mfumo wa serikali
hizi mbili tuna matatizo mawili… la kwanza, unaona kabisa kuna hali
fulani ya misuguano ya kimadaraka na ndio inajenga kitu kama chuki au
kutoridhika dhidi ya upande mwingine, ukienda kwa upande wa Znz wanayo
mambo mengi dhidi ya upande wa bara na ukienda kwa Wabara nao wana mambo
mengi wanayolalamikIa dhidi ya Wazanzibari, kama hatujatatua hayo
katika serikali mbili, serikali ya tatu haiwezi kutatua, ndio
itayazidisha’
6. ‘Nikupe mfano hai, Zanzibar
wana wimbo wa taifa, Rais wao, bunge lao wana serikali yao na Rais wao
anapigiwa mizinga 21 kama Rais wa Jamuhuri ya muungano, zamani hayo
hayakuepo yamekuja taratibu tu ndio maana nasema kama kuna mvutano flani
hivi’
7. ‘Hayo katika mfumo huu wa
serikali mbili ungeweza kusema hayapendezi sana….. sasa utakapoweka
serikali ya tatu ya Tanganyika, inamaanisha Tanganyika itakua na wimbo
wake wa taifa, serikali yake, bunge lake, wimbo wake wa taifa, Rais wake
pia atapigiwa mizinga 21…… yani kule Zanzibar Rais wake anapigiwa
mizinga 21, huku anapigiwa mizinga 21, na huyu unaemuita bwana mkubwa
anapigiwa mizinga 21′
Hayo ndio maoni ya Frederick Sumaye aliekua waziri mkuu wa Jamuhuri
ya muungano wa Tanzania kwenye awamu ya tatu iliyoongozwa na Benjamin
Mkapa.
Credit:millardayo
Friday, 24 January 2014
MAMBO 7 ALIYOYASEMA FREDERICK SUMAYE KUHUSU SERIKALI TATU NA KATIBA MPYA. .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment