Find Us On Facebook
 
X

Monday 27 January 2014

MOURINHO: ILIKUWA VIGUMU KUMWACHIA MATA

Juan Mata na Mzee Mourinho
Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinhoamesmea kuwa ulikuwa ni 'uamuzi mgumu' kwake kumwachilia mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya Uhispania Juan Mata kujiunga na wapinzani wao katika ligi kuu ya England Manchester United.
Mata aliye na umri wa miaka, 25, ameandikisha rekodi ya uhamisho katika klabu ya Man United kwa baada ya kuuzwa na Chelsea kwa kititia kinono cha pauni milioni 37.1.
Akizungumza na BBC Mourinho amesema:
" Haya ni maamuzi ambaye mkufunzi anapaswa kufanya, lakini kwangu ilikuwa vigumu. Ningependa kuendelea kumwona katika kikosi changu bila shaka,"
Juan Mata na mkufunzi David Moyes wa Man United

0 comments:

Post a Comment