Find Us On Facebook
 
X

Sunday 12 January 2014

MAN UNITED YAZINDUKA, YAICHAPA 2-0 SWANSEA CITY

KOCHA David Moyes amepumua
kidogo baada ya Manchester United
kushinda 2-0 dhidi ya Swansea City
usiku huu Uwanja wa Old Trafford na
kuepuka kipigo cha nne mfululizo na
cha tatu Uwanja wa nyumbani.
Ushindi wa United leo katika mchezo
huo wa Ligi Kuu ya England
umetokana na mabao ya Antonio
Valencia dakika ya 47 na Dany
Welebeck dakika ya 59
United sasa inatimiza pointi 37 baada
ya kucheza mechi 21, ingawa inabaki
nafasi ya saba kwenye msimamo.

0 comments:

Post a Comment