Find Us On Facebook
 
X

Sunday 12 January 2014

MAN CITY YAREJEA KILELENI LIGI KUU ENGLAND, MWAKA HUU KAZI IPO

MABAO ya Edin Dzeko na Alvaro
Negredo yametosha kuipa ushindi wa
2-0 Manchester City dhidi ya
Newcastle Uwanja wa St James Park
na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu
England.
Nyota wa Bosnia alifunga bao la
kwanza dakika ya nane akiunganisha
krosi ya Aleksandar Kolarov
kumtungua kipa Tim Krul.
Kikosi cha Alan Pardew kilidhani
kimepata bao la kusawazisha baada
ya shuti la mbali la Cheick Tiote
kumpita kipa Joe Hart na kutinga
nyavuni, lakini likakataliwa kwa
sababu Yoan Gouffran alikuwa
ameotea.
Negredo akaifungia City bao la pili
dakika za majeruhi. Ushindi huo
unaifanya City irejee kileleni baada ya
kutimiza pointi 47 kutokana na mechi
21, ikiishusha Chelsea yenye pointi 46
baada ya kucheza mechi 21 pia katika
nafasi ya pili. Arsenal sasa ni ya tatu
kwa pointi zake 45, ingawa imecheza
mechi 20.

0 comments:

Post a Comment