Kuna
siku nilikua napiga stori na baadhi ya watu wangu wa nguvu ambao
wamefanikiwa kufika Nigeria na kujionea jinsi kiwanda cha muziki wa huko
kilivyo na taratibu zake ambazo wanaona ni tofauti na za nchi kama
Tanzania, mastaa wa muziki ni wengi na kazi za kibalozi kwenye makampuni
makubwa kama ya simu ni sehemu ya wanakopata mamilioni kila siku.
Waliniambia kampuni moja ya mawasiliano ya simu za mkononi inaweza
kuwa na mabalozi hata watano ambao wote ni wasanii wa muziki hivyo
inatoa fursa tofauti na nchi nyingine ambako akishapewa hilo dili msanii
mmoja ndio mpaka amalize muda wake na nchi nyingi
hawawatumii/hawatambui umuhimu wa kuwatumia Mastaa.
Wanigeria pia wameweza kuvuka mipaka mpaka kwenye mauzo ya nyimbo
zao, nakumbuka siku moja nikiwa South Africa nilikutanishwa na Mnigeria
ambae anamiliki kampuni inayouza nyimbo za Wanigeria kwenye kampuni
zinazotengeneza simu za mkononi kama vile Samsung, yani ukinunua simu
mpya tu ukiingia kwenye videoz na songs unakuta nyimbo za Wasanii wa
Naija.
Baada ya hayo maelezo machache hapo juu naomba kukufahamisha kwamba
picha hiyo ya kwanza ni ya magari matatu yanayomilikiwa na mastaa wa
Nigeria, magari haya yote matatu yamepigwa picha yakiwa yamepaki sehemu
moja.
Producer aliemtoa D’Banj >> Don Jazzy anaiendesha hiyo Aston
Martin, Wizkid anaiendesha hiyo Porsche wakati D’Prince anaisukuma hiyo
Mercedes Benz.
Katika stori kadhaa ambazo nimewahi kuzipokea, Mastaa wa Nigeria,
Congo DRC, South Africa na Uganda ndio naona utajiri wao unaridhisha
Afrika.
Sunday, 12 January 2014
MAGARI MATATU YA MASTAA WA NIGERIA KWENYE PICHA MOJA, WIZKID, D PRINCE NA DON JAZZY.
Sunday, January 12, 2014
No comments
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment