Elifrida
Nicholaus (6), mkazi wa Mkolani, Nyamagana jijini hapa alizaliwa mzima
kabisa lakini sasa ni kilema baada ya kudaiwa kuchomwa moto mkononi na
shangazi yake aliyemtaja kwa jina moja la Esta.
Mtoto Elifrida Nicholaus baada ya kuchomwa moto na shangazi yake.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea
Julai 10, mwaka jana ambapo Elifrida aliyechukuliwa kutoka Kigoma kwa
wazazi wake na kwenda kuishi Mkolani jijini hapa kwa shangazi yake,
alijikuta akiambulia mateso makubwa yalimsababishia kupoteza vidole
vyake vya mkono wa kulia kwa kuchomwa moto.
Akielezea jinsi ilivyokuwa, Elifrida
ambaye kwa sasa analelewa katika kituo cha watoto waliofanyiwa ukatili
cha Foundation alisema kwa uchungu:
“Nakumbuka siku hiyo shangazi alinifunga
mikono na miguu kwa kamba na kuuzungushia mkono wake kipande cha
godoro na kunifunga kwa ‘nailoni’ kisha akaniwasha moto mpaka moto
ulipoisha, alinichia baada ya mimi kupiga makelele ya maumivu.”
Mkono wa Elifrida Nicholaus baada ya kuunguzwa.
Shangazi yake huyo alifikishwa kituo cha
polisi cha Igogo, Nyamagana na kupewa fomu ya PF-3 ambapo alipelekwa
Hospitali ya Wilaya ya Sengerema kwenye kitengo cha watu walioungua na
moto kisha akapatiwa matibabu ambapo alilazimika kukatwa vidole vyake
vilivyoathirika vibaya huku vingine vikiongezewa nyama aliyokatwa
kutoka mapajani.
Akizungumza na waandishi wetu, mama wa
Elifrida aliyejitambulisha kwa jina la Malina Fabian alisema anaomba
msaada wa kisheria kwa kuwa kesi ya mtoto wake inachukua muda mrefu.
‘’Naomba jamani taasisi inayohusika na
sheria ishughulikie kesi ya mtoto wangu kuharakisha maana ni muda mrefu
sasa,’’ alisema mama wa mtoto huyo.
Awali, kesi ya mtoto huyo ilitakiwa
kutajwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana mwishoni mwa mwaka jana
lakini ilisemekana haikutajwa kutokana na sababu zisizofahamika ndipo
tume ya haki za binadamu ilipoingilia kati kwa ajili ya kusikilizwa
upya mahakamani hapo.
credit:vituko vya mtaa
0 comments:
Post a Comment