Wachezaji mashuhuri katika ligi za soka za Uingereza na zile za
Brazil wanajiunga na kampeni ya kuwaonya mashabiki dhidi ya kuwatumia
makahaba watoto wakati wa michuano ya kombe la dunia nchini Brazil
baadaye mwaka huu.
Wachezaji wa klabu ya Chelsea Frank Lampard,Oscar na Ramirez wanaunga
mkono kampeni hiyo inayoshirikisha kitengo cha kukabiliana na uhalifu
nchini Uingereza pamoja na serikali ya Brazil.
Kampeni hiyo inawaonya wafuasi wa Uingereza kwamba watakabiliwa na
tisho la kushtakiwa iwapo watalipa ili kulala na wasichana walio chini
ya umri 18.
Taifa la Brazil linakadiriwa kuwa na nusu ya milioni ya idadi
makahaba watoto wanaosimamiwa na na magenge ya uhalifu na kuna hofu
kwamba idadi hiyo itaongezeka wakati wa michuano hiyo.
Kufuatia hatua hiyo serikali ya Brazil imeanzisha kampeni kwa
kushirikiana na wachezaji mashuhuri kupinga biashara ya ukahaba kwa
wasichana wadogo kiumri.
Thursday, 6 February 2014
Wachezaji hawa waunga mkono kampeni ya ukahaba kwa watoto nchini Brazil
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment