Huyu ndio mwafrika pekee kutoka katika nchi ya Afrika Magharibi –
Cameroon ambaye amewahi kuvaa jezi ya klabu ya Manchester United.
Eric Djemba Djemba, kiungo mkabaji wa timu ya taifa ya Cameroon ‘The
Indomitable Lions’, alipata bahati kubwa ya kuweza kusajiliwa na
Manchester United mnamo mwaka 2003 akitokea klabu ya Nantes ya Ufaransa
kwa ada ya uhamisho ya paundi million 3, alisajiliwa akitajwa kuja kuwa
mrithi wa kiungo mahiri Roy Keane lakini baada ya muda mfupi tu
alishindwa kufikia malengo kwa kuendekeza starehe na kushindwa kufanya
kazi iliyompeleka Old Trafford.
Mwisho wa siku mcameroon huyo akauzwa kwenda Aston Villa ambapo napo
alishindwa kung’ara na kuanza taratibu kupotea katika ulimwengu wa soka
la kiwango cha juu.
Lakini baada ya kupotea kwa muda muda mrefu wiki hii kiungo huyo
ambaye alifilisika amepata bahati ya kusajiliwa na timu St. Mirren
inayoshiriki kwenye ligi kuu ya Scotland.
Djemba mabaye kwa sasa ana umri wa miaka 32, pia amewahi kuvichezea
vilabu vya Odense na Burnley baada ya kutoka Aston Villa kabla ya kwenda
Qatar na kisha Urusi.
Friday, 7 February 2014
FAHAMU ALIPO MCAMEROON HUYU PEKEE ALIYEWAHI KUICHEZEA MAN UNITED
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment