Find Us On Facebook
 
X

Friday 7 February 2014

HUU NDIO MSHAHARA ANAOLIPWA MBWANA SAMATTA TP MAZEMBE.

sam

Kwenye kumbukumbu miaka minne iliyopita mshambuliaji toka Tanzania anayeichezea Tp Mazembe ya DR Congo Mbwana Ally Samatta hakuwahi kumake headline katika soka hapa nyumbani zaidi ya kusikika kwa mbali wakati akiitumikia timu yake ya African Lyon.
smt
African Lyon kwa kipindi hiko ilikuwa ikimilikiwa na mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji au Mo ambapo kwa kipindi hicho ilikuwa ikipambana kupanda Ligi Kuu Tanzania Bara kwa muda huo Samatta hakuwa maarufu lakini kwa aina ya uchezaji wake na msaada mkubwa kwa timu yake,taratibu jina likaanza kupanda.
Msimu mmoja tu baada ya kushiriki Ligi Kuu Bara Dewji aliamua kuiuza timu hiyo na baadaye Samatta alijiunga na club ya Simba ambayo aliitumikia kwa msimu mmoja tu kabla ya kuuzwa TP Mazembe ya DR Congo.
Unaambiwa kwa sasa Samatta ni mmoja kati ya wachezaji ghali barani Afrika na ndiye anayesemekana kulipwa vizuri kuliko wachezaji wengine wanaocheza soka kutoka Tanzania bila ya kujali wako bara la Afrika,Asia au Ulaya.
Kwa sasa Mshahara wa Samatta na TP Mazembe kwa mwezi ni dola 10,000  kwa Tanzania ni zaidi ya Sh milioni 16 maana yake mshahara wake unaweza kuwalipa wachezaji wa timu moja ya Ligi Kuu Bara kwa mwezi.
Mfano ni timu za jeshi kama JKT Ruvu,Ruvu Shooting,JKT Oljoro na nyinginezo,lakini timu kama Ashanti ni kati ya zile ambazo mshahara wa mwezi wa Samatta unaweza kuwalipa wachezaji wao kwa asilimia 90 au 100 kabisa.
Lakini mshahara pekee hautoshi kuonyesha mabadiliko ya haraka sana ya Samatta, vitu vingine vikubwa viwili ni thamani anayopewa kwa kipindi hiki kuwa imefikia dola pauni 450,000 (zaidi ya Sh bilioni 1.2).
Taarifa ikifikie kuwa hakuna mchezaji wa Tanzania ambaye aliwekwa kwenye soko kupitia mitandao maarufu ya mauzo ya wanasoka na akafikia thamani ya Samatta na ili kuonyesha kuwa thamani yake,Klabu ya Al Ain inayoshiriki Ligi Kuu ya Falme za Kiarabu ((UAE)unaambiwa iko tayari kutoa dola milioni 1 (zaidi ya Sh bilioni 1.6) ili kumnasa Samatta akacheze kwenye timu yao.
Source:Salehjembe.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment