Find Us On Facebook
 
X

Friday 7 February 2014

TAFADHALI SOMA SIMULIZI HII:-MWANDISHI LIYEJINYONGA BAADA YA KUPOKEA TUZO....INAUMIZA SANA






Mwandishi liyejinyonga baada ya kupokea tuzo....Inaumiza sana

Picha hii inamwonyesha binti mdogo wa kisudani akiwa ananyemelewa na ndege mla nyama aina ya tai.
Binti huyu alianguka njiani baada ya kushindwa kuhimili njaa kali iliyokiwa imembana na alikuwa akielekea katika kituo cha msaada wa chakula.
Tai huyo mla nyama za viumbe hai alimla mtoto huyo na ndio ukawa mwisho wa uhai wake uliomkuta akiwa njiani kuelekea kuokoa uhai wake.
Picha hii ilipigwa na mwandishi wa habari aitwaye Kevin Carter na Kwa mara ya kwanza ilichapishwa kwenye gazeti tarehe 26 March mwaka 1993.
Pia na kupitia picha hii Carter alishinda tuzo ya Pulitzer Prize mwaka 1994.
Miezi michache baada ya kuchukua zawadi ya Pulitzer, Carter
alikutwa akiwa amejiua kwa kuumia kwa kitendo cha kinyama alichokifanya na watu wengi nchini Afrika ya kusini walimlaumu kwa picha hiyo.
Carter alikimbilia kuichukua picha na kusahau kuwa pamoja na yeye kuwa mwanahabari lakini pia alikiwa na jukumu la kuokoa uhai wa binti huyu na mwishoni kuacha mtoto aliwe huku yeye akishuhudia.
Ndugu zangu, pamoja na kazi zetu tufanyazo tunatakiwa kufikia kipindi na kuwa na roho za utu na kuheshimu na kuwapenda binadamu wenzetu.
Kila unyama mtu unaoufanya sasa kwa binadamu mwenzako kumbuka mateso yake ni kukosa amani na mwishowe hata kujikuta ukiyachukua maamuzi kama ya Carter.
Hebu kumbuka katika maisha yako umefanya mangapi kwa makusudi na kuhatarisha maisha ya mwenzako?
Je unatambua kuwa kila binadamu ana haki ya kuishi na wewe ukiwa mmoja wapo na kusaidia mwenzako aishi?
Mungu atupe mioyo ya upendo na kuwajali wenzetu tukiamini ya kuwa tunafuraha hivi kwa kuwa tunawaona binadamu wenzetu na kama wasipokuwepo kuna uwezekano mkubwa wa kuwa maisha yetu hayana maana.
Comment R.I.P kwa binti aliyekufa na kisha share kuwakumbusha watu juu ya kupendana katika dunia hii.

0 comments:

Post a Comment