Find Us On Facebook
 
X

Thursday 27 February 2014

The Game aweka wazi kuhusu uhusiano wake na Kim & Khloe Kardashian

gameKhloe Kardashian na The game walijiachia pamoja kwenye night club kiasi cha kuwapa watu mashaka kwamba  wawili hao wapo kwenye uhusiano wa kimapenzi hivi sasa.
Khloe alikuwa wa kwanza kukanusha uhusiano huo na kusema kwamba walikuwa wapo kwenye starehe kama marafiki.
Hivi karibuni The game amepata nafasi ya kuzungumzia kuhusu kile kilichotokea na ametoa exclusive mpya.
Akiwa kwenye radio ya BBC Radio1 Extra The game alisema asingeweza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Khloe kwasababu alikuwa na uhusiano na dada yake Kim kipindi kilichopita.
“Watu hawajui kuhusu mimi na Khloe kwamba tumejuana miaka 12 iliyopita. Nilikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Kim Kardashian kwa muda kidogo sana. Kanye West alikuwa bado mshkaji kipindi kile na hadi sasa bado ni mshkaji wangu na najua Kim anakaribia kuwa mke wake na tayari wanafamilia. Khloe pia ni mshkaji na tuko poa pamoja kwa hiyo hizo tetesi  kati yangu na Khloe hazina ukweli”
k

Maneno ya Diamond Platnumz kuhusu wasanii wanaomtengenezea ugomvi

Screen Shot 2014-02-27 at 9.37.36 AM

Staa huyu wa ‘Number 1 rmx’ ft Davido ameiandika hii na kuisambaza kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ya Instagram na facebook.
Screen Shot 2014-02-27 at 9.36.11 AM

Ex-girlfriend wa Samuel Eto’o ashtua watu kuhusu umri wa mchezaji huyo.

hu
“Tatizo la Chelsea ni kukosa wafungaji, nina Eto’o ambaye ana miaka 32 au labda 35 nani anayejua?”.
Hiyo ilikua ni kauli ya kocha Jose Mourinho akimzungumzia Samuel Etoo na baadae mpenzi wa zamani wa Eto’o aliongea kuhusu umri wa mchezaji huyo kitu ambacho kimewashangaza watu wengi.
Anna Barranca alikuwa mpenzi wa zamani wa Eto’o na kupata mtoto mmoja wa kike ambaye hivi sasa ana miaka 11 amesema Eto’o ana miaka 39 kuelekea 40 na sio 35.
Mwanamke huyo amesema kwamba alijua kuhusu umri wa Eto’o wakati wapo Cameroon kutoka kwa mtu ambaye alikua pamoja na Etoo tangu utotoni.

P Square kuanzisha series yao mpya – The Alingo’s

2
Project hii imefanyiwa kazi kwa muda wa miaka 5 na mwaka huu ipo tayari kuanza kuonyeshwa, taarifa hii imetoka kwenye post ya Peter Okoye.
The Alingo’s ni TV series ya katuni ambayo stars wake ni Peter na Paul wakiwa kwenye muonekano wa katuni.
Project hiyo inasimamiwa na P Classic entertainment kampuni ambayo ipo chini ya P Square na kuongozwa na Peter Okoye.
Hii ni trailer ya series hiyo

Trailer....

Taarifa kuhusu kocha wa Taifa Stars kuachishwa kazi

Kim-PoulsenShirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen wamekubaliana kuvunja mkataba katika makubaliano ambayo ni siri kwa pande zote mbili.
Uamuzi huo umetangazwa leo (Februari 27 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kwa pamoja na Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Kocha Poulsen mbele ya waandishi wa habari.
Rais Malinzi kwa niaba ya TFF ametoa shukrani za dhati kwa Kocha Poulsen kwa ushirikiano na mchango ambao ameutoa kwa Tanzania kuanzia kwenye mpira wa miguu wa vijana.
Naye Kim amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi cha miaka mitatu alichokaa nchini kuanzia Mei 2011 alipoteuliwa kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana, na baadaye Taifa Stars.
Akizungumzia benchi jipya la ufundi la Taifa Stars, Rais Malinzi amesema linatarajiwa kutangazwa hivi karibuni likiongozwa na kocha kutoka nje ya Tanzania.
Amesema kwa upande wa mechi dhidi ya Namibia itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Stars itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi akisaidiwa na kocha Hafidh Badru kutoka Zanzibar.
Katika hatua nyingine, Kocha Madadi amewaondoa wachezaji watano wa Yanga katika kikosi kilichotajwa awali ili wapate fursa ya kuitumikia timu yao kwenye mechi mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Ahly ya Misri.
Wachezaji hao ni Athuman Idd, David Luhende, Deogratius Munishi, Frank Domayo, Kelvin Yondani na Mrisho Ngasa. Pia kipa Ivo Mapunda ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kupata msiba.
Nafasi zao zimezibwa na wachezaji Abdi Banda (Coastal Union), Himid Mao (Azam), Juma Luizio (Mtibwa Sugar), Said Moradi (Azam) na Shabani Kado (Coastal Union).
Taifa Stars itaingia kambini keshokutwa (Machi 1 mwaka huu) jioni kwenye hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam, na itaondoka Machi 3 mwaka huu alfajiri kwa ndege ya South African Airways na kurejea nchini Machi 7 mwaka huu saa 8.15 mchana.

Wednesday 26 February 2014

Video inayosambaa ya Ostaz Juma akiombwa msamaha na Pnc.

21
Hii ni video ambayo imezunguka sana leo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ambayo wadau wengi wa muziki wamedai ni kama kudharirishwa kwa wasanii wa Tanzania na kuonekana kama hawana msimamo na kazi yao waifanyayo.
31
Video hii inamunyesha memba wa zamani wa kundi hilo la Mtanashati Intertainment Pnc,akimuomba msamaha Big boss wa kundi hilo Ostaz Juma Namusoma.




Hii ndiyo status ya Kala Jeremiah iliyozua utata Facebook.

kalaa
Kwa kitu ambacho kinaonekana si cha kawaida kwa Kala Jeremiah kuandika status kali ikiwa kama inamchafua Diamond na kumsifia Ally Kiba kwa kile kilichosemekana kuwa Ally Kiba kakopa pesa ili kumalizia ujenzi wa nyumba aliyokuwa anajenga.
Screenshot_2014-02-26-13-09-30

Friday 14 February 2014

MAITI ZAKUTWA ZIMETELEKEZWA MUHUNGULA KAHAMA,TUNAOMBA RADHI KWA PICHA

Maiti zimekutwa zikiwa zimeteketea vibaya mjini kahama maeneo ya mhungula sababu ya maiti hizo bado ikiwa haijafahamika ni nini.



chanzo http://bundalawilliam.blogspot.com

MAGAZETI YA LEO VALENTINE DAY


.
.

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
mg16-w480-h580
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.