Jana jioni kupitia mshindi wa shindano la vipaji la BSS 2013 Emmanuel Msuya aliziachia picha za nyumba aliyonunua, gari pamoja na studio… vyote akiwa kavifanya kutokana na zile milioni 50 za ushindi wa BSS.
Yafuatayo ni maoni ya Nay wa Mitego ambae aliwahi kudiss kwenye wimbo wake kwamba washindi wa BSS pesa za ushindi wanapewa, mbona hakionekani chochote?
Ya moyoni kutoka kwa Ney ni haya >>> ‘kitu ambacho watu walikua hawajui ni kwamba hivyo vitu alivyokua akivifanya mimi ni mtu wa kwanza kunieleza, aliposhinda tu ile November 30 2013 alinipigia simu siku ya pili akajitambulisha kwa kusema ‘brother mimi ni Emmanuel Msuya mshindi wa BSS, nakukubalia sana’
‘Nimefurahi kusikia hivyo na ni moja kati ya vitu ambavyo huwa naviimba, hii ni nzuri zaidi… hiki ndicho kinachotakiwa kufanywa’ -Nay
credit:millardayo
0 comments:
Post a Comment