
1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)
Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American
alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi
kuwa na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya Yesu
yalikuwa sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi
sana ambayo mtu yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa
maarufu hata zaidi yake...