majonziTaarifa zilizotoka muda mfupi uliopita kuhusiana na zoezi la utafutaji wa ndege iliyopotea ya AirAsia QZ 8501 zinasema kuwa vikosi vinavyohusika na utafutaji wa ndege hiyo vinasema kuna uwezekano mkubwa imezama kwenye kina kirefu cha bahari. Chanzo cha habari kutoka nchini humo kinasema uchunguzi kuhusu ndege hiyo bado unaendelea huku wakitumia ndege za kijeshi kutoka Indonesia na Singapore Kusini Magharibi mwa Pwani ya Borneo ambapo ilipoteza mawasiliano. kapt Rubani wa ndege hiyo Captain Iriyanto Bado jitihada za kuwatafuta abiria 162 waliokuwepo ndani ya ndege zinaendelea,na mpaka sasa hakuna mawasiliano yoyote,ilikua ikielekea Singapore. Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia na shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung. air
Monday, 29 December 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment