Find Us On Facebook
 
X

Tuesday, 30 December 2014

Utafiti kuhusu athari za chumvi kwenye chakula .

Moja ya vitu ambavyo vimekuwa muhimu kwenye chakula cha mwanadamu ni chumvi ambayo hutumika kuongeza ladha ya chakula ambacho hutumika mezani . Umuhimu wa kiungo hiki umefikia hatua ya waswahili kuipbatiza chumvi jina la utani ambalo ni Mkuu Wa Jiko . Hata hivyo chumvi inaweza kuwa na madhara pale ambapo inatumika kuliko kawaida na madhara hayo ni kwa afya ya mtumiaji . Je chumvi ni mbaya kwa Afya yako? Mwili wa mwanadamu unahitaji chumvi kwa kiwango Fulani kwani inasaidia kuongeza mnadini ambayo mwili wako unayahitaji . Hatari ni pale unapokula chumvi nyingi kuliko kiwango ambacho mwili wako unahitaji . Imagundulika kuwa chumvi husababisha matatizo ya shinikioz la damu hali ambayo inaweza ikaongeza uwezekano wa mtu kupata matatizo ya shambulio la moyo pamoja na hatari nyingine za magonjwa ya moyo . Madaktari wanashauri utumiaji wa chumvi kwa kiwango cha chini ili kuepukana na matatizo haya . salt on food Je kiasi gani cha chumvi kinazidi kiwango cha kawaida . Kimsingi hupaswi kula zaidi ya gramu tano za chumvi kwa siku , hii ni sawa na kijiko kimoja cha chai ambacho kina ujazo wa milligram 5 . Kiwango hiki kinajumuisha chumvi ambayo unaongeza ukiwa unapika jikoni , chumvi unayoongeza mezani wakati wa kula na ile chumvi ambayo inapatikana kwneye chakula kiasili hii ni kwa sababu kuna vyakula ambavyo ndani yake kuna chumvi hata kama havina ladha ya chumvi . Mfano wa vyakula ambavyo tayari vina chumvi ndani yake ni Mikate , Sausage na nyama za kusaga , supu ya kutengenezwa kiwandani , vyakula vya nafaka ambavyo hutumika kwenye kifungua kinywa (breakfast) n ahata baadhi ya biskuti . Je tunatumia chumvi nyingi kuliko kawaida ? Waafrika wengi huwa na kasumba ya utumiaji wa chumvi kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida na hii imezoeleka sana kuanzia majumbani mpaka mahotelini . Ni rahisi sana kutumia chumvi nyingi kuliko kawaida wakati wa milo ya kila siku . Nusu ya chumvi ambayo hutumiwa na watu ni chumvi inayopatikana kwenye vyakula hasa vile vya kutengenezwa viwandani ambayo huwekwa wakati wa utengenezaji wa vyakula hivi huko huko viwandani ili kuvifanya vikae kwa muda mrefu . Nusu nyingine ni ile ambayo ambayo huongezwa jikoni na ile ambayo watu huongeza mezani wakati wa kula ili kukoleza ladha ya chakula husika . Salt_Farmers_-_Pak_Thale-edit1 Nini kinatengeneza chumvi Chumvi inatengenezwa na vitu viwili ambavyo ni sodium na chloride , Sodium ni sehemu ya chumvi ambayo ambayo huongeza presha ya damu au kwa lugha inayoeleweka zaidi huongeza shinikizo au msukumo wa damu hasa pale unapotumia chumvi nyingi kuliko kiwango cha kawaida . Pamoja na ukweli kwamba tunatumia chumvi nyumbani , taarifa zinaoandikwa kwenye vihifadhi vya vyakula hasa vile ambavyo vinatengenezwa viwandani huonyesha kiwango cha madini ya sodium ambayo yametumika kwenye chumvi . Kijiko kimoja cha chai mara nyingi huwa kina miligramu 2000 za sodium . Ni jinsi gani tunaweza kutumia kiwango cha chini cha chumvi kwenye vyakula ? Haiwezekani kupunguza kiwango cha chumvi ndani ya siku moja au ghafla , mabadiliko yanapaswa kufanyika hatua moja baada ya nyingine . Muhimu ni kujizoesha hisia ya kudhani kuwa chakula kina ladha hata pale ambapo chumvi haijakolea Kama una kawaida ya kuongeza chumvi nyingi mezani hatua ya kwanza ni kuondoa kile kikopo kidogo cha chumvi mezani hasa wakati wa chakula , hii ni kwa sababu unapaswa kukumbuka kuwa kama ulishaongeza chumvi tangu jikoni hauna sababu ya kuongeza nyingine mezani . MSHARIQEN-7612-1 Jaribu pia kupunguza kiwango cha chumvi unachoongeza wakati wa mapishi yako , unapswa kuonja wakati ukiwa unapika ili kuepuka kuongeza kiwango cha chumvi ambcho kinaweza kuwa hatari kwa Afya yako . Kama chakula chako kina viungo ambavyo ndani yake kuna chumvi ya asili hupaswi kuongeza chumvi nyingine juu yake . Katika tafiti zilizofanyika hivi karibuni imefahamika kuwa kuna baadhi ya vitu vinavyoweza kutumika kama chuimvi ambavyo havna madhara sawa na ya chumvi kwenye mwili wa mwanadamu na mojawapo ni limao pamoja na ndimu . Kiungo kingine kinachoweza kuchukua nafasi ya chumvi kwenye chakula chako ni mdalasini . salt Vyakula visivyo na chumvi nyingi? Vyakula ambavyo havijatengenezwa kiwandani kwa maana ya vyakula halisi mara nyingi huwa havina chumvi nyingi na hii inamaanisha kuwa unapaswa kuchagua vyakula vya asili kuliko vile ambavyo vimetengenezwa viwandani . o-SALT-SHAKER-facebook

Monday, 29 December 2014

Keith Millen meneja wa Crystal Palace?

Kocha wa muda wa timu Crystal Palace Keith Millen yuko tayari kuchukua jukumu la kuifundisha timu hiyo kama kocha wa kudumu. Millen anakaimu nafasi ya umeneja kwa muda baada ya kocha mkuu Neil Warnock kutimuliwa ,amekua na uzoefu wa kukiongoza kikosi hicho baada ya kufanya hivyo mara ya kwanza ni pale Tony Pulis alipoikacha timu hiyo mwanzoni mwa msimu. "Niko tayari kuwa kocha wa kudumu wachezaji wananiheshimu kwa ufahamu wangu, na kufanya kazi kwa bidii nimefanya hivi mara kadhaa pamoja nao". Pia kumekua na tetesi kocha Alan Pardew anaweza pewa nafasi ya kuwa kocha mpya katika klabu hiyo ya kusini mwa londoni.

Taarifa ya kinachoendelea hivi sasa kuhusu ndege iliyopotea jana Indonesia

majonziTaarifa zilizotoka muda mfupi uliopita kuhusiana na zoezi la utafutaji wa ndege iliyopotea ya AirAsia QZ 8501 zinasema kuwa vikosi vinavyohusika na utafutaji wa ndege hiyo vinasema kuna uwezekano mkubwa imezama kwenye kina kirefu cha bahari. Chanzo cha habari kutoka nchini humo kinasema uchunguzi kuhusu ndege hiyo bado unaendelea huku wakitumia ndege za kijeshi kutoka Indonesia na Singapore Kusini Magharibi mwa Pwani ya Borneo ambapo ilipoteza mawasiliano. kapt Rubani wa ndege hiyo Captain Iriyanto Bado jitihada za kuwatafuta abiria 162 waliokuwepo ndani ya ndege zinaendelea,na mpaka sasa hakuna mawasiliano yoyote,ilikua ikielekea Singapore. Shughuli ya kutafuta ndege ya AirAsia ambayo ilipotea jana Jumapili imeendelea leo tena baada ya kusitishwa kwa muda. Ndege hiyo ilikuwa safarini kwenda nchini Singapore ikitokea mji wa Surubaya nchini Indonesia na shughuli za kuitafua zinafanyika kwenye kisiwa cha Belitung. air

Hili ni dili analofungia mwaka 2014 msanii Davido

DavidO (1)Mwezi December ni mwezi ambao watu huwa wanafanya uchambuzi wa namna mwaka ulivyokwenda, kuangalia malengo ambayo umeyaweka yamepita au yamekwama na pia kuandaa mikakati mipya ya mwaka unaofuatia. Davido ni mmoja ya mastaa wanaomaliza vizuri 2014, amefanya vizuri kwenye muziki, siku ya December 27 alitoka na tuzo mbili kwenye AFRIMA Awards 2014, msanii Bora wa Mwaka na pia Hit Single yake ya ‘Aye’ kuwa wimbo bora wa mwaka. “JUST SIGNED A DEAL WITH CLOSE UP! GREAT WAY TO END THE YEAR!! NON STOP THANK YOU LORD!! #owonikoko”– @davidoofficial Hizo ni dalili njema kwa Davido 2015, tayari amesign dili ya kutangaza dawa ya mswaki ya Close Up, kasema ina mavuno ya Naira nyingi hivyo mbali na mauzo ya album aliyopanga kuitoa mwakani pamoja na deal nyingine ikiwemo ya shows, kupitia hii kajihakikishia mkwanja wa kutosha 2015.

Wakati wengine wakisherehekea kupata watoto…hali si shwari kwenye ndoa ya mchekeshaji maarufu Chris Rock

Wakati wengine wakisherehekea kupata watoto…hali si shwari kwenye ndoa ya mchekeshaji maarufu Chris Rock Posted by: Jesca TZA December 29, 2014 Ent. FILE: Comedian Chris Rock Has Filed For Divorce From Malaak Compton-RockMchekeshaji maarufu nchini Marekani Chris Rock ameamua kuachana na mpenzi wake wa siku nyingi Malaak Campton baada ya kudumu nae kwenye ndoa kwa miaka 19. Katika maelezo yaliyotolewa na mkewe Malaak alisema “baada ya mgongano mrefu na kudumu kwa miaka 19 katika ndoa yetu,Chris na mimi tumeamua kutengana na kila mmoja kufanya mambo yake”. rokMwanasheria wa mchekeshaji huyo Robert S.Cohen alithibitisha kupokea barua ya talaka toka kwa Kris kwenda kwa mkewe Malaak na kusema haya ni mambo binafsi na wahusika wameamua kuyafanya kwa usiri ili kulinda heshima ya watoto wao,”alisema Mwanasheria huyo katika moja ya jarida la nchini humo.