WAKATI
ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume huwarubuni wanafunzi
wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za kielimu kutokana na
kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako mwanafunzi wa
Kidato cha Pili anadaiwa kumzalisha mwalimu wake.
Mwanafunzi
huyo aliyemzalisha mwalimu wake ana umri wa miaka 17, wakati mwalimu
huyo anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya Umma ya Nkasi, iliyopo
mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, Rukwa, ana umri wa miaka 25.
Tukio hilo linalotajwa kuwa la kwanza kutokea wilayani hapa, limekuwa gumzo kubwa kwa wakazi wa Nkasi na wilaya jirani.
Hata
hivyo, kwa wanafunzi, wamekuwa wakimpongeza mwenzao kwa kujaliwa kupata
mtoto katika umri wake huo mdogo, huku mzazi mwenzake akiwa na uhakika
wa maisha kutokana na kuwa ni mtumishi serikalini.
Imeelezwa
kuwa licha ya tukio hilo, mwalimu huyo aliyezaa na mwanafunzi wake bado
anaendelea na masomo shuleni hapo, huku `mzazi’ huyo wa kiume
akifundishwa na mzazi mwenzake.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mjini Namanyere hivi karibuni, Mkuu wa
Shule ya Sekondari Nkasi mjini Namanyere ambayo ni ya mchanganyiko ya
umma, Amiamie Nanga alisema mwalimu huyo alianza kazi shuleni hapo ikiwa
ni mara yake ya kwanza kufundisha baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu
chuoni.
“Yameshatokea, lakini haileti picha nzuri sana, lakini mimi nina
uzoefu mkubwa na wakazi wa mwambao wa Ziwa Tanganyika, kwao si ajabu
kuwa na uhusiano na watu waliowazidi umri, iwe kwa mtoto wa kike au wa
kiume, wote ni sawa tu…
“Lakini
katika kisa hiki, inaonesha walimu sasa wanapoteza haiba ya ualimu. Hii
kazi ina miiko na maadili yake …kwa mwalimu huyu hii ni ajira yake ya
kwanza, nikimaanisha ni kituo chake cha kwanza cha kazi tangu ahitimu
masomo yake…” alisema.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema hakuna kosa kwa mwalimu huyo wa kike kwa kuwa tayari ni mtu mzima.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema hakuna kosa kwa mwalimu huyo wa kike kwa kuwa tayari ni mtu mzima.
“Isitoshe katika kisa hiki ni nadra kumpata mlalamikaji … Mwalimu
mwenyewe huyu wa kike hawezi kuwa tayari kujidhalilisha kuwa amebakwa,
yalikuwa maamuzi yake.”
Aliongeza
kuwa, kwa mwalimu huyo kupata ujauzito wa mwanafunzi wake hakuwezi
kuathiri ajira yake, tofauti na mwalimu wa kiume akimpatia ujauzito
mwanafunzi wake wa kike ambaye huathirika kwa kukatisha masomo.
Jitihada
za kumpata mwalimu huyo wa kike na mwanafunzi huyo zimegonga mwamba
baada ya watu wao wa karibu kumweleza mwandishi kuwa hawako tayari
kuuzungumzia mkasa huo.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule hiyo waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi kwa
masharti ya kutoandikwa majina yao kwa hofu ya kuchukuliwa hatua za
kinidhamu shuleni hapo, pamoja na kukiri kutambua uhusiano baina ya
mwanafunzi mwenzao na mwalimu wao, lakini walisema hivi sasa mwalimu
huyo amesitisha uhusiano na mwenzao na kuanzisha uhusiano mpya na
mwalimu mwenzao.
Walisema
pamoja na mambo mengine ni kama mwanafunzi mwenzao ameathirika
kisaikolojia baada ya ‘kupinduliwa’ na mwalimu wake wa kiume ambaye kwa
sasa ndiye baba mlezi wa mtoto.
“Huyu
mwalimu wa kike sisi sasa tunamwita shemeji yetu alikuwa na uhusiano wa
kimapenzi na mwenzetu… penzi lao lilikolea hadi sasa ameweza kumzalia
mtoto huyo…, lakini kwa sasa inavyoelezwa ni kwamba penzi limehamia kwa
mwalimu mwenzake,“ alisema mmoja wao.
Baadhi
ya watu wa karibu na mwanafunzi huyo wanakiri kuwa mwanafunzi huyo hana
uwezo wa kifedha kumudu kumpatia malezi stahiki mtoto wake huyo, hivyo
hata mzazi mwenzake alipoanza uhusiano na mwalimu mwenzake hakuwa na
jinsi, bali kukubaliana na matokeo.
“Usiniandike jina, sisi tunashauri mwalimu huyo wa kike na mpenzi
wake huyo wa kiume ambaye ni mwalimu mwenzake wahamishiwe shule nyingine
kwa sababu kama kioo katika jamii wameteleza kwa kiasi kikubwa na
watashindwa kuwajenga na kuwalea wanafunzi wao kimaadili.
“Isitoshe
tunajiuliza sheria hapa inasemaje maana kama angekuwa ni mwalimu wa
kiume amempatia mwanafunzi wake wa kike ujauzito angeshitakiwa na
kufikishwa mahakamani na pengine kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka
30 jela, sasa kwa hili sheria inasemaje?”Alihoji.
Baadhi
ya wazazi mkoani hapa waliohojiwa na mwandishi kwa nyakati tofauti
wameelezea kushangazwa na tukio hilo, na hasa kwa jinsi mwalimu
alivyoshindwa kujizuia `kujiachia’ kimapenzi kwa mwanafunzi wake.
Credit: Habarileo
Credit: Habarileo
0 comments:
Post a Comment