Find Us On Facebook
 
X

Tuesday 7 October 2014

KUHUSU OKWI KUPATA MAJERAHA

IMG_7819.JPG
Zikiwa zimebaki takribani mbili kabla ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga, daktari wa Simba SC, Yassin Gembe amesema kwamba mshambuliaji, Mganda Emmanuel Okwi aligongwa kwenye enka na goti katika mchezo dhidi ya Stand United, lakini yuko fiti kabisa kucheza Oktoba 18, dhidi ya Yanga SC.
Okwi alitolewa nje mara mbili kupatiwa huduma ya kwanza na Dk Gembe, lakini mara zote alirejea uwanjani kuendelea na mchezo.
Pigo la pili lilimfanya mchezaji huyo aendelee kucheza huku akichechemea, hali ambayo ilizua hofu labda amepata maumivu makubwa.
“Ni kweli Okwi aligongwa mara mbili,
mara moja kwenye enka na mara moja
kwenye goti. Lakini hayakuwa maumivu makubwa na ataendelea na mazoezi na wenzake” amesema Gembe
Aidha, Dk Gembe amesema kwamba
kipa Ivo Mapunda na beki Nassor
Masoud ‘Chollo’ wataanza mazoezi ya
kujiweka fiti wiki hii.
Ivo aliumia kidole na anatakiwa kuwa
nje kwa wiki nane, hivi sasa akiwa
yupo katika wiki ya tatu, wakati Chollo
aliyeumia mkono, anatakiwa kuwa nje
kwa wiki tatu, hivi sasa akiwa
anaingia katika wiki ya pili.
“Hawa wachezaji maumivu yao
hayawazuii kufanya mazoezi ya
kujiweka fiti, kwa hivyo niliwapa
mapumziko mafupi kabla ya kuanza
mazoezi ya kukimbia na gym. Ivo
nilimpa wiki mbili za kupumzika na
Chollo wiki moja, kwa hivyo wote wiki
hii wataanza mazoezi,” Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ na Haroun
Chanongo ambao wiki iliyopita
walifanya mazoezi mepesi, nao
wataanza mazoezi kikamilifu na
wenzao.
Majeruhi mwingine wa muda mrefu
Simba SC ni Mkenya, Paul Kiongera
ambaye anatakiwa kuwa nje kwa wiki
sita baada ya kuumia goti, hivi sasa
akiwa katika wiki ya nne- na Dk
Gembe amesema ‘fowadi’ huyo
anaendelea vizuri.

Monday 6 October 2014

MWANAFUNZI WA MIAKA 17 AMTUNDIKA MIMBA MWALIMU WAKE HUKO MKOANI RUKWA

WAKATI ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume huwarubuni wanafunzi wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za kielimu kutokana na kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako mwanafunzi wa Kidato cha Pili anadaiwa kumzalisha mwalimu wake.
 
Mwanafunzi huyo aliyemzalisha mwalimu wake ana umri wa miaka 17, wakati mwalimu huyo anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya Umma ya Nkasi, iliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, Rukwa, ana umri wa miaka 25.
 
Tukio hilo linalotajwa kuwa la kwanza kutokea wilayani hapa, limekuwa gumzo kubwa kwa wakazi wa Nkasi na wilaya jirani.
 
Hata hivyo, kwa wanafunzi, wamekuwa wakimpongeza mwenzao kwa kujaliwa kupata mtoto katika umri wake huo mdogo, huku mzazi mwenzake akiwa na uhakika wa maisha kutokana na kuwa ni mtumishi serikalini.
 
Imeelezwa kuwa licha ya tukio hilo, mwalimu huyo aliyezaa na mwanafunzi wake bado anaendelea na masomo shuleni hapo, huku `mzazi’ huyo wa kiume akifundishwa na mzazi mwenzake.
 
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Namanyere hivi karibuni, Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkasi mjini Namanyere ambayo ni ya mchanganyiko ya umma, Amiamie Nanga alisema mwalimu huyo alianza kazi shuleni hapo ikiwa ni mara yake ya kwanza kufundisha baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu chuoni.
 
“Yameshatokea, lakini haileti picha nzuri sana, lakini mimi nina uzoefu mkubwa na wakazi wa mwambao wa Ziwa Tanganyika, kwao si ajabu kuwa na uhusiano na watu waliowazidi umri, iwe kwa mtoto wa kike au wa kiume, wote ni sawa tu…
 
“Lakini katika kisa hiki, inaonesha walimu sasa wanapoteza haiba ya ualimu. Hii kazi ina miiko na maadili yake …kwa mwalimu huyu hii ni ajira yake ya kwanza, nikimaanisha ni kituo chake cha kwanza cha kazi tangu ahitimu masomo yake…” alisema.
  
 Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema hakuna kosa kwa mwalimu huyo wa kike kwa kuwa tayari ni mtu mzima.
 
“Isitoshe katika kisa hiki ni nadra kumpata mlalamikaji … Mwalimu mwenyewe huyu wa kike hawezi kuwa tayari kujidhalilisha kuwa amebakwa, yalikuwa maamuzi yake.”
 
Aliongeza kuwa, kwa mwalimu huyo kupata ujauzito wa mwanafunzi wake hakuwezi kuathiri ajira yake, tofauti na mwalimu wa kiume akimpatia ujauzito mwanafunzi wake wa kike ambaye huathirika kwa kukatisha masomo.
 
Jitihada za kumpata mwalimu huyo wa kike na mwanafunzi huyo zimegonga mwamba baada ya watu wao wa karibu kumweleza  mwandishi  kuwa hawako tayari kuuzungumzia mkasa huo.
 
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi kwa masharti ya kutoandikwa majina yao  kwa hofu ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu shuleni hapo, pamoja na kukiri kutambua uhusiano baina ya mwanafunzi mwenzao na mwalimu wao, lakini walisema hivi sasa mwalimu huyo amesitisha uhusiano na mwenzao na kuanzisha uhusiano mpya na mwalimu mwenzao.
 
Walisema pamoja na mambo mengine ni kama mwanafunzi mwenzao ameathirika kisaikolojia baada ya ‘kupinduliwa’ na mwalimu wake wa kiume ambaye kwa sasa ndiye baba mlezi wa mtoto.
 
“Huyu mwalimu wa kike sisi sasa tunamwita shemeji yetu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwenzetu… penzi lao lilikolea hadi sasa ameweza kumzalia mtoto huyo…, lakini kwa sasa inavyoelezwa ni kwamba penzi limehamia kwa mwalimu mwenzake,“ alisema mmoja wao.
 
Baadhi ya watu wa karibu na mwanafunzi huyo wanakiri kuwa mwanafunzi huyo hana uwezo wa kifedha kumudu kumpatia malezi stahiki mtoto wake huyo, hivyo hata mzazi mwenzake alipoanza uhusiano na mwalimu mwenzake hakuwa na jinsi, bali kukubaliana na matokeo.
 
“Usiniandike jina, sisi tunashauri mwalimu huyo wa kike na mpenzi wake huyo wa kiume ambaye ni mwalimu mwenzake wahamishiwe shule nyingine kwa sababu kama kioo katika jamii wameteleza kwa kiasi kikubwa na watashindwa kuwajenga na kuwalea wanafunzi wao kimaadili.
 
“Isitoshe tunajiuliza sheria hapa inasemaje maana kama angekuwa ni mwalimu wa kiume amempatia mwanafunzi wake wa kike ujauzito angeshitakiwa na kufikishwa mahakamani na pengine kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka 30 jela, sasa kwa hili sheria inasemaje?”Alihoji.
 
Baadhi ya wazazi mkoani hapa waliohojiwa na mwandishi kwa nyakati tofauti wameelezea kushangazwa na tukio hilo, na hasa kwa jinsi mwalimu alivyoshindwa kujizuia `kujiachia’ kimapenzi kwa mwanafunzi wake.

Credit: Habarileo

Rekodi 7 tofauti alizoweka Cristiano Ronaldo baada ya kufunga hat trick dhidi ya Bilbao

10649779_808787392518541_1971687263503280706_nMwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo jana usiku alifunga magoli matatu na kutimiza jumla ya magoli 17 katika michuano yote aliyoitumikia Real Madrid.
Magoli hayo yalimfanya Ronaldo aweke rekodi kadhaa kwenye historia ya soka na rekodi hizo zipo kama ifuatavyo:
*3 – Hii ni Hat trick ya 3 ya Ronaldo katika La Liga msimu huu na amefanikiwa kufunga hat tricks hizo katika kipindi cha siku 15 tu.
*111 – Mchezo wa jana usiku ulikuwa wa 111 kwa Ronaldo kuitumikia timu yake ya taifa au klabu na katika mechi hiz zote amefunga zaidi ya goli moja.
*Cristiano amekuwa mchezaji wa pili kufunga hat tricks 3 katika mechi 7 za raundi ya kwanza ya La Liga – baada ya Mariano Martin kufanya hivyo msimu wa 1943-44.
*Cristiano ndio mchezaji wa kwanza kufunga magoli 13 au zaidi katika mechi 7 za kwanza Liga – tangu alipofanya hivyo Echevaria katika msimu wa 1943. 
*50 – Cristiano Ronaldo mpaka sasa ameshatoa assists 50 kwa wachezaji wenzie wa Real Madrid.
*190 – Magoli matatu aliyofunga Cristiano Ronaldo jana dhidi ya Athletic Bilbao yalimfanya atimize jumla ya magoli 190 katika mechi 171 alizoichezea Real Madrid kwenye ligi.
*9 – Gareth Bale mpaka sasa amempa Cristiano Ronaldo assists nyingi kwenye La liga tangu mwanzo mwa msimu uliopita – amempata assists 9.

Abakwa akimtembeza Mbwa