Find Us On Facebook
 
X

Tuesday 8 July 2014

Kuhusu kuachiwa kwa filamu hii mpya kutoka nigeria

yello
Bodi ya filamu nchini Nigeria hatimaye imeidhinishwa kusambazwa kwa sehemu kubwa na kuonyeshwa kwa filamu hii kubwa barani Afrika Half of a Yellow Sun.
Awali Half of a Yellow Sun ilicheleweshwa na bodi hiyo na kufafanua sababu za kufanya hivyo kuwa ni kutokana na hali ya usalama inayoendelea katika nchi hiyo na kusema kuwa filamu hiyo inayoelezea vita vya wenyewe kwa wenyewe Nigeria ingeweza kusababisha machafuko.
yelo
Filamu hiyo kitabu chake kiliandikwa na mwandishi mahiri wa vitabu Chimamanda Adichie,
Hatua hiyo imekuja kipindi ambacho watengenezaji wa filamu hiyo ya Half Of A Yellow Sun tayari kuwa wameorodhesha kwa ajili ya kuonyeshwa nchini Marekani.

Kuhusu kipa Ochoa wa Mexico kuwa na vidole sita

BqWzg71CIAAhaGC
Katika michuano ya kombe la dunia kumeibuka wachezaji wengi ambao wameonyesha uwezo mkubwa kiasi cha kuteka hisia za watu wengi, mmoja wapo ni golikipa wa Mexico Guillermo Ochoa.
Golikipa huyu alionyesha uwezo mkubwa katika mechi alizoichezea Mexico kwenye michuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini Brazil, kabla ya timu yake kutolewa na Uholanzi katika hatua 16 bora – lakini pamoja na kuondolewa kwa timu yake bado uwezo wake umeacha gumzo kubwa sana kwenye michuano hii.
Uwezo aliouonyesha Ochoa ulipelekea kuzuka kwa taarifa kwamba golikipa huyo wa Mexico aliumbwa akiwa na vidole sita vya mkononi. Zikatolewa mpaka picha kupitia vyombo vya habari mbalimbali ambavyo vilimuonyesha Ochoa akiwa na vidole sita.
06042250-f68e-11e3-b3a2-3503811abc43_AP962717263961
Lakini ukweli ni kwamba kipa huyo ambaye kwa sasa anawindwa na vilabu vingi hana vidole sita. Picha zilizoonyeshwa na kusambazwa kwenye vyombo vya habari ni za kutengeneza.